loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nabi ataka mabao mengi Yanga

Nabi ataka mabao mengi Yanga

ZIMEBAKI siku tano kabla ya Yanga kuikabili Rivers United ya Nigeria, kocha mkuu wa timu hiyo,  Nasriddine Nabi amesema kazi kubwa anayoifanya hivi sasa ni kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji ili kuweza kufunga mabao mengi zaidi.

Yanga na Simba zinaliwakilisha taifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Azam FC na Biashara United zenyewe zinapeperusha bendera ya Tanzania kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza kwa niaba ya kocha Nabi, Meneja wa Yanga Hafidhi Salehe alisema maandalizi yao yamekamilika kwa kiasi kikubwa na anachokifanya kocha hivi sasa ni kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ili kuzitumia nafasi wanazotengeneza.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri tangu kumalizika wiki ya kilele cha Wananchi, tumefanya mazoezi ya kutosha na mechi mbili za kirafiki ambazo zimenisaidia kupata picha halisi ya kikosi changu hasa katika mchezo uliombele yetu karibu idara zote zipo sawa ulinzi na hata kiungo ispokuwa bado kuna kitu nataka kuongeza kwenye umaliziaji lengo ni kufunga mabao mengi zaidi,” alisema Nabi.

Kocha huyo alikiri kutowajua vizuri wapinzani wao Rivers United, lakini alisema maandalizi waliyofanya yanampa matumaini ya kushinda mchezo huo sababu hata wachezaji wameonesha kujituma na kuwa na shauku ya kupata matokeo.

Kocha huyo raia wa Tunisia alisema anaridhishwa na uwezo wa washambuliaji wake wote, Fiston Mayele, Heritier Makambo na Yacouba Sogne kwa namna wanavyojituma, lakini angependa wazidi kujituma zaidi na kuzitumia ipasavyo kila nafasi wanayopata ili kuumaliza mchezo huo mapema kabla ya kwenda Nigeria.

Yanga imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu uliopita nyuma ya bingwa Simba, ambayo nayo itaanzia kwenye mzunguko wa kwanza baada ya msimu uliopita kuishia hatua ya robo fainali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/37fc1351d2699af17d173dda0dba3f53.jpg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: Mohammed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi