loader
Dstv Habarileo  Mobile
Changamoto kambi ya Azam Zambia

Changamoto kambi ya Azam Zambia

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam FC, wamerejea kutoka Zambia huku `wakilia’ na baadhi ya changamoto zilizojitokeza  katika kambi hiyo ya siku 12.

Msemaji wa timu hiyo, Thabit Zakaria alisema jana kuwa timu hiyo ilicheza mechi tatu za majaribio nchini humo.

“Timu yetu jana (juzi) iliondoka Ndola, Zambia kwa Shirika la Ndege la Kenya kupitia Nairobi na tulifika Nairobi saa 9 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na tulianza safari ya kurudi Dar es Salaam saa 5 usiku, ” alisema Zakaria.

Alisema licha ya kambi hiyo, lakini kuna mambo hayakwenda sawa, hivyo kulikuwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kuwakosa baadhi ya wachezaji wao nyota, hasa wale wanaocheza timu zao za taifa, ambazo zilikuwa na mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia.

 ‘’Kambi yetu ilitarajia kuwa na wachezaji 29, lakini tukajikuta kwa muda  mrefu tukiwa na wachezaji 19, hiyo ikiwa na maana kuwa kambi yetu iliwakosa wachezaji 10, ambapo wengi waliitwa katika timu zao za taifa, “alisema.

’’Taifa Stars imetoa wachezaji saba katika timu yetu. Kenya na zingine nazo zilichukua wachezaji, pia tulimkosa nahodha wetu Aggrey Morris ambaye ni majeruhi, hiyo ni changamoto nyingine, “alisema Zakaria.

Alisema kuwa hata mazoezi yao ya Dar es Salaam wataendelea na wachezaji walionao, na kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Horseed ya Somalia Jumamosi Uwanja wa Azam Complex.

Timu hizo zitarudiana tena baada ya wiki moja kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Wakati wa kambi hiyo nchini Zambia, Azam ilicheza mechi tatu, na kufungwa 4-0 dhidi ya Arrows kabla ya kuifunga Kabwe Warriors kwa bao 1-0 na kushinda tena idadi kama hiyo dhidi ya Zesco United.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f0865cb293b83b3165469c688f163eeb.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Na Amina Jumanne, TUDARCo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi