loader
Timu 16 kucheza Ligi Kuu Zanzibar

Timu 16 kucheza Ligi Kuu Zanzibar

JUMLA ya timu 16 zinatarajiwa kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu wa mwaka 2021/2022, imeelezwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuongezeka kwa timu nne zilizopanda daraja msimu huu badala ya mbili, ambazo kwa mujibu wa kanuni zilitakiwa kupanda awali.

Katika kanuni msimu wa 2020/2021, timu mbili zilitakiwa kushuka, moja kutoka kila upande, lakini msimu huu zimeongezeka timu nne na kupanda timu sita na kufanya idadi ya timu 16.

Hivyo katika ongezeko la timu hiyo, timu nne zilizopanda ni kutoka Kisiwani Pemba na mbili kutoka Unguja, ambapo kwa timu za Pemba ni Yosso Boys, Dortmund, Selem View na Machomane, ambazo zilipatikana baada ya  kucheza michezo ya Play Off iliyomalizika juzi.

Pemba timu nne zilizopanda zilipatikana kwa kucheza mtoano maalumu, ambao ulishirikisha timu nane za juu zilizocheza Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Pemba.

Timu hizo zilizoshiriki hatua hiyo ni Mwenge, Chipukizi, New Stone Town,  Selem View, Wawi Star, Machomanne, Yosso Boys na Dortmund.

Timu nyingine ambazo zitashiriki Ligi Kuu Zanzibar kutoka Unguja ni mabingwa watetezi KMKM, Zimamoto, KVZ, Mafunzo, JKU, Kipanga, Malindi, Mlandege, Polisi, Black Sailors, Uhamiaji na Taifa ya Jang'ombe.

Hivyo ili kuepuka uwepo wa ligi mbili ndipo Serikali ilipotangaza kuchezwe ligi itakayokuwa na timu 16 badala ya 12 ambazo mbili zilipanda kutoka Unguja Uhamiaji na Taifa ya Jang’ombe na nne kutoka Pemba.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/2d9939c34c54e14448cd4a1d42b572ee.jpg

KLABU ya Simba imegomea kuvaa nembo ...

foto
Mwandishi:  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi