loader
39,000 kupewa Sh 4,000 kukabili Covid-19

39,000 kupewa Sh 4,000 kukabili Covid-19

WAFANYAKAZI 39,000 wa sekta ya utalii katika maeneo ya ukanda wa pwani, watapatiwa Sh 4,000 kila mmoja kila mwezi katika miezi mitatu ili kuwawezesha kukabiliana na athari za Covid-19.

Chama cha Utalii Pwani ya Kenya (KCTA), kilisema takribani wafanyakazi 39,000 watapatiwa Sh milioni 600 katika mpango wa miezi mitatu.

Fedha hizo zinatokana na makubaliano kati ya KCTA na taasisi isiyo ya kiserikali ya Give Direct ili kunufaisha waliopoteza ajira, katika sekta ya hoteli na kwamba, wanaolengwa ni wafanyakazi waliopoteza ajira au waliopunguzwa mshahara kutokana na kupungua kwa mapato yatokanayo na utalii.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa KCTA, Julius Owino, alisema kila mmoja kati ya wafanyakazi hao 39,000 atapatiwa fedha taslimu Sh 4,000 kila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu.

"Mwanzoni tulifikiria kununua vitu kama sabuni kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta ya utalii, lakini tuligundua mahitaji yanatofautiana hivyo kuamua kuwapatia fedha taslimu katika wiki mbili hadi tatu zijazo na hii itafanywa kila mwezi kwa miezi mitatu,” alisema Owino.

Alitoa mwito kwa serikali za kaunti sita za Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River, Taita Taveta na Lamu zinazolengwa na mpango huo, kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa chanjo kukabiliana na Covid-19 kutokana na kuwa mstari wa mbele katika utoaji huduma

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/32a2531475ea8f8b91553e871116277b.jpg

MGANDA Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia katika ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi