loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali kujenga masoko ya kisasa 12

Serikali kujenga masoko ya kisasa 12

SERIKALI inatarajia kuanza ujenzi wa masoko mengine 12 ya kisasa 12 katika Mwaka wa Fedha wa 2021/2022 katika manispaa mpya nchini yakijumuishwa na masoko mapya mengine 14 ambayo ama yamekamilika, au ujenzi unaendelea katika hatua mbalimbali.

Manispaa hizo 14 ni Arua, Entebbe, Fort Portal Gulu, Hoima, Jinja, Kabale, Lira, Masaka, Mbale, Mbarara, Moroto, Soroti na Tororo ambazo zilinufaika na mradi wa kwanza wa Dola za Marekani milioni 150 (sawa na Sh bilioni 527) kutoka Benki ya Dunia.

Waziri wa Serikali za Mitaa, Raphael Magyezi, alisema baadhi ya wilaya zitakazonufaika na mradi ni pamoja na Gomba, Kakumiro, Kikuube, Kyankwanzi, Kyotera,

Lwengo, Mubende, Rakai, Sembabule na kwamba, kila soko litagharimu kati ya Sh bilioni 15 na bilioni 25 kulingana na ukubwa.

Alisema mbali na ujenzi wa masoko, pia serikali imepanga kujenga vituo vya kisasa vya burudani, maeneo ya magari ya kukodi na vituo vya mabasi katika serikali za mitaa.

Waziri Magyezi alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, halmashauri za miji 300 zitapata fedha kuanza kufanya kazi katika mazingira bora kwa sababu ya mipango madhuubuti iliyopo wizarani na katika serikali kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Mipango (NPPB), Amanda Ngabirano, alisema: "Tunahitaji msaada wa kisiasa katika juhudi za bodi ili kuongeza kufuata na utekelezaji wa mipango ya kisheria ya maendeleo ya miji, hasa kutoka kwa wanasiasa wanaoshindwa kupanga mipango kwenye  miji vizuri," alisema.

Alisema serikali imetoa Sh bilioni 4.5 kwa NPPB kuhakikisha kuwa kuna mipango sahihi katika vituo vya miji nchini, kwa kuanzia na miji 11 nchini kote katika mwaka huu wa fedha.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/2f72ca91996a0926f97cd05b4fe62310.jpg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi