loader
Uganda, Sudan Kusini zaafikiana doria

Uganda, Sudan Kusini zaafikiana doria

NCHI za Uganda na Sudan Kusini zimekubaliana kufanya doria katika Barabara Kuu ya Nimule-Juba ambapo madereva na wasafiri wamekuwa wakishambuliwa katika siku za hivi karibuni.

Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Uganda, Rebecca Kadaga aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa ‘twitter’ kwamba, kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa polisi kila baada ya kilomita 10 kando ya barabara kuu hiyo yenye shughuli nyingi.

"Uganda imeelezea wasiwasi wake kwa kuendelea kushambuliwa na kuuawa kwa wasafiri wa Uganda katika Tarafa ya Juba-Nimule.

Makubaliano hayo yameafikiwa na Serikali ya Sudan Kusini kuanzisha doria za usalama katika kila baada ya kilomita 10 inayolindwa na wasindikizaji wa msafara," aliandika.

Kadaga alisema wakuu wa wafanyakazi kutoka nchi hizo mbili watafanya mkutano wa pamoja wiki hii.

"Nimewavutia wenzangu pia kwa ukiukaji wa kawaida wa Itifaki ya Soko la Pamoja na Serikali ya Sudan Kusini," ameongeza.

Wiki iliyopita, madereva wa kuvuka mpaka kutoka nchi za Afrika Mashariki waligoma kupita katika barabara hiyo kwa ukosefu wa usalama.

Karibu malori 1,000 kutoka nchi za Afrika Mashariki yote yamesimama katika sehemu kuu ya kuvuka kando ya barabara Kuu ya Nimule-Juba.

Takribani wafanyabiashara na madereva wa lori 30 kutoka Afrika Mashariki wameuawa mwaka huu katika barabara hiyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3776c3b5e794a022e501d342214c12e3.jpg

MGANDA Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia katika ...

foto
Mwandishi: Sudan Kusin

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi