loader
Dstv Habarileo  Mobile
Joyce Kiria ataka uwekezaji kwa wanawake

Joyce Kiria ataka uwekezaji kwa wanawake

MWANAHARAKATI wa masuala ya wanawake nchini, Joyce Kiria amewataka wanawake wajasiriamali kuwekeza zaidi katika ubunifu wa kazi zao kwa kuziongezea thamani zaidi ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.

Joyce alitoa mwito huo wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali wa Kata ya Yombo Vituka waliojitokeza kwenye semina ya siku moja aliyowaandalia kupitia mradi wake wa Wanawake Live, semina hiyo inalenga kuwawezesha kiuchumi wanawake kwa kuwapatia elimu ya biashara ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuunga mkono harakati za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua wanawake kiuchumi.

Joyce aliwataka wanawake hao kufahamu kuwa kujituma na kuwa wabunifu katika ufanyaji biashara zao ikiwa pamoja na nidhamu ya kazi ndiyo msingi mkubwa katika kujiinua kimaisha.

Alisema:”Wanawake wenzangu ninaomba mfahamu kuwa kamwe Rais Samia hatokuja kufungua pochi zetu na kuweka fedha isipokuwa amehakikisha serikali yake inaweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara kwetu ili tuyatumie mazingira hayo kujiongezea kipato,
Rais Samia ameonesha nia ya kutuinua wanawake na ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunajituma na ndiyo maana na mimi mwanamke mwenzenu ninakuja kuwaelimisha mbinu za biashara nikishirikiana na Diwani wenu na wataalamu wengine ili kunufaika na sera za Rais Samia za kutuinua.”

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Yombo Vituka, Fulgence Lwiza aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, aliwataka wanawake kufahamu kuwa serikali inatambua nafasi yao katika kukuza uchumi na ndiyo maana imerahisisha upatikanaji wa mikopo isiyokuwa na riba kupitia Halmashauri huku akiwataka kufuatilia mikopo hiyo Halmshauri ya Temeke.
Alisema kuwa sera nzuri za serikali za kusaidia wanawake zitakuwa na tija zaidi iwapo wanawake wenyewe wakizichangamkia hasa kwa kufanya shughuli za kukuza uchumi wao ambao ndiyo chachu ya kukuza uchumi wa  nchi kwa ujumla.

“Mfahamu kuwa serikali imeshusha mfumo mzuri wa kusaidia wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya taifa hadi mtaa na siye ndiyo wasimamizi wa sera hizo, sasa ninatumia wasaha huu kuwasihi wanawake mjitume na kuhakikisha mnanufaika na sera hizi nzuri za nchi” alisema Diwani huyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/57962b6557119cadd9b6339dbc3e86ef.jpg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: Na Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi