loader
Dstv Habarileo  Mobile
Stars yajikita kileleni

Stars yajikita kileleni

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaongoza msimamo wa Kundi J, ikiwa na pointi nne, baada ya leo kushinda mchezo wake wa pili kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa mabao 3-2 katika Uwanja wa Mkapa.

Mabao ya Taifa Stars yamefugwa na Erasto Nyoni dakika ya pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Simon Msuva kufanyiwa madhambi eneo la hatari, mabao mengine yalifungwa na Novatus Morish dakika ya 26, na Feisal Salum dakika 52.

Mabo ya Madagascar yalifungwa na Njiwa Rakotoharimalala na Thomas Fountaine kwa mpira wa adhabu ndani ya eneo la hatari.

Baada ya ushind huo, Taifa Stars imekijita kileleni mwa msimamo huo, ikiwa na pointi sawa na Benin, kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, baada ya kushinda mchezo wa leo na kutoa sare dhidi ya DR Congo wiki iliyopita.

Benin inashika nafasi ya pili, DR Congo inashika nafasi ya tatu na Madagascar anaburuza mkia. Oktoba 6, 2021 Taifa Stars atacheza dhidi ya Benin na DR Congo itacheza dhidi ya Madagascar.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/444d5d9fc36975db0c8d58f9bf2fc196.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi