loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanzania leo kushawishi  uwekezaji kilimo biashara

Tanzania leo kushawishi uwekezaji kilimo biashara

WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, leo anatarajiwa kuongoza jopo la Watanzania kushawishi uwekezaji katika kilimo biashara kwenye mkutano mkubwa wa kilimo Afrika unaofanyika Nairobi , Kenya.

Mkutano huo uliofunguliwa jana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta unajadili mifumo ya chakula na unashirikisha nchi 11 zenye miradi ya kilimo ya Shirika la Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA).

Hayo yalielezwa katika mkutano kati ya waandishi wa habari wakiwemo maofisa habari wa serikali kutoka wizara mtambuka kwenye sekta ya kilimo na taasisi ya AGRA ikishirikkiana na SAGCOT uliofanyika Dar es Salaam jana.

Viongozi wengine wanaotarajiwa katika mkutano huo wa Jukwaa la Mapinduzi ya kijani Afrika (AGRF), ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Siza Tumbo na Balozi wa Tanzania China, Mbelwa Kairuki.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga alisema katika mkutano huo Tanzania ina nafasi kubwa ya kuonesha vipaumbele vyake kuvutia wawekezaji katika kilimo biashara.

Katika tukio hilo litakalovutia watu zaidi ya 10,000 duniani Tanzania itaelezea utayari wake katika kushirikiana na wawekezaji katika kilimo biashara.

Hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo wakati akizindua Chumba cha Majadiliano Kilimo-Biashara 2021 alisema serikali inataka kuongeza mauzo ya mazao ya kilimo katika soko la kimataifa hivyo itashiriki katika mkutano wa Nairobi kwa nia hiyo.

Alisema kwa kutanua soko hilo kutasaidia wakulima wa Tanzania kupata faida zaidi katika kilimo chao na taifa kunufaika kwa pato la kigeni.

“Kila kitu tunachozalisha katika kilimo kinatakiwa mahali fulani duniani,” alisema Profesa Tumbo. Mwakilishi wa AGRA nchini, Donald Mizambwa alisema Tanzania ambayo kwa sasa ni miongoni mwa nchi chache zinazojitosheleza kwa chakula ina fursa nyingi za kilimo biashara ambazo zinatakiwa kujulikana na wadau wengine duniani ili wazishiriki.

Kirenga alizungumzia masoko na kusema ili watanzania wawe na uhakika wa soko ni lazima waongeze tija ili yeyote anayetaka bidhaa nchini Tanzania awe na uhakika wa kupata kipindi chote cha mwaka katika ubora unaotakiwa.

“Hii itasaidia kuwa na uhakika wa soko tusipokuwa na tija hatutakuwa na soko,” alisema Kirenga. Katika mkutano huo pia washiriki wa Tanzania watawasilisha mahitaji yao na kuona ni namna gani wenye mitaji wanaweza kusaidia kuimarisha zaidi kilimo biashara nchini .

Kilimo cha Tanzania kwa sasa kinajiweka vyema katika ramani ya dunia kutokana na uratibu wa maendeleo ya kilimo kupitia mpango wa ASDP ll.

Lengo jingine la jukwaa la AGRF mwaka huu ni kuhakikisha Afrika inakuwa na sauti moja kuhusiana na mifumo ya chakula na kuweka sauti moja katika mkutano ujao wa Umoja

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/20226d3c0e38d4d88ef57b418fa52c51.jpg

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi