loader
Yanga yakimbilia Fifa

Yanga yakimbilia Fifa

KLABU ya Yanga imekimbilia Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu baada ya nyota wake watatu wa kigeni kuwa katika hatihati ya kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria Jumapili.

Yanga inaikaribisha timu hiyo ya Nigeria katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali utkaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumzia jana Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara aliwataja wachezaji hao kuwa ni Khalid Aucho, Shaban Djuma na Fiston Mayele na sababu kubwa ni kuchelewa kwa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).

Alisema kilichotokea Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kwa mujibu wa taratibu zao wakasema muda umeshapita na baada ya mashauriano waliandika barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) na kuelezwa kuwa Aucho yupo huru, ingawa Wamisri walizuia kibali chake.

Kwa mujibu wa Manara, Aucho alikuwa na mgogoro na klabu yake, Mayele na Djuma mikataba yao ilikuwa inaisha Agosti 31, mwaka huu.

“Kukosekana kwa wachezaji hawa haikuwa makosa ya klabu, sisi tulipeleka maombi ya ITC DR Congo pale tu tulipoingia mkataba, wakasema subirini mpaka tarehe 31, tukawaeleza inawezekana vipi wakati muda wa dirisha utakuwa umeshafungwa,”

“Kukawa na ushindani mkubwa sana, tulipeleka mapema wakashindwa kutupa ITC kwa wakati, wakatoa siku moja baada ya dirisha kufungwa,”

Manara alisema waliwasiliana na Caf kuhusu wachezaji wote watatu ila hawakutoa majibu na sasa wanasubiri barua ya Fifa kuona uwezekano wa kutoa ITC hizo kabla ya mchezo huo.

Alisema kukosekana kwa wachezaji hao ni pengo kwa sababu ni wazuri ila wamefanya usajili wa kikosi kipana hivyo, waliopo ana imani watafanya vizuri.

Kuhusu mchezo huo ujao, alisema wachezaji wameonesha ari kwenye timu na wako tayari kwa mchezo, huku akitaja kauli mbiu yao kuwa ni Mabingwa Wamerejea akisema ni timu ya kwanza Afrika Mashariki kucheza michuano hiyo miaka ya zamani na kufika hatua ya makundi na robo fainali.

Alisema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanachukua mataji yote ya Ligi, Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho (FA), Mapinduzi na ikiwezekana ubingwa wa Afrika.

Alisema Yanga itakwenda uwanjani siku hiyo ikiwa tofauti kupigania jezi yao na kuwakilisha vyema Taifa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c128693a9782849725085a67feecbb8b.jpeg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi