loader
SERIKALI YAIPA STARS MILIONI 10/-

SERIKALI YAIPA STARS MILIONI 10/-

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa Sh milioni 10 kwa timu ta taifa, Taifa Stars, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia Qatar 2022.

Akizungumza baada ya mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam juzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa alisema Wizara imetoa fedha hizo kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wa Stars.

’’Kikosi cha Taifa Stars kitapewa bonasi ya Sh milioni 10 kama zawadi itakayotoa motisha ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mechi za kufuzu fainali ya Kombe la Dunia, ’’ alisema Bashungwa.

Bashungwa pia amewapongeza vijana wa timu ya Taifa Stars na Watanzania wote kwa ujumla kwa ushindi huo, ambao unaifanya timu hiyo kuongoza katika Kundi J, ambalo mbali na Madagascar, lina timu za Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR).

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa watanzania wote wadau wa michezo wenye zawadi kwa timu ya Taifa Stars, kuwasiliana na wizara yake ili kuwatia hamasa wachezaji wa timu hiyo.

Kwa ushindi huo wa juzi, Taifa Stars imefikisha pointi nne na kuongoza kundi lake katika mbio hizo za kusaka nafasi ya kwenda Qatar, ambapo Afrika itatoa timu tano.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/43a4218ab7860efaeebb9dbd7b12ebfe.jpeg

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine ...

foto
Mwandishi: Amina Jumanne, TUDARCo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi