loader
Yanga hatihati kucheza bila mashabiki Dar

Yanga hatihati kucheza bila mashabiki Dar

WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika mashindano ya kimataifa wako katika hatihati ya kucheza bila mashabi-ki baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kukataza mashabiki katika mechi zao.

Timu ambazo zina mechi mwezi huu ni Yanga ambao wanacheza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya  River United ya Nigeria utakaochezwa kesho kutwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Biashara United na Azam FC ambao wanacheza Kombe la Shirikisho Afrika, ambao wanacheza leo.

Biashara United wataivaa Dikhil FC ya Djibouti ugenini leo na Azam FC watacheza na Horseed ya Somalia kesho nyumbani.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo alisema ni kweli Caf imezuia mashabiki viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona lakini TFF imeomba angalau waruhusiwe mashabiki kiasi lakini bado hawajajibiwa.

“Ni kweli Caf imezuia mashabiki viwanjani lakini TFF haijakaa kimya imeliandikia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) angalau mashabiki kiasi waruhusiwe lakini hadi sasa hatujajibiwa na endapo hatutajibiwa mechi zote zitachezwa bila mashabiki,” alisema Ndimbo.

Alisema mashabiki wasiwe na hofu kwani bado TFF inapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha wanapata kibali lakini ikishindikana basi maana hata mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Madagascar wa kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar waliomba lakini hawakuruhusiwa.

Azam FC ambao watacheza kesho Uwanja wa Azam Complex, kupitia kwa msemaji wao, Zakaria Thabit tayari wamethibitisha kuwa hawatacheza na mashabiki kwa sababu Caf wamekataza.

Yanga ambao nao watacheza Jumapili Uwanja wa Mkapa huenda nao wakacheza bila mashabiki endapo TFF watakuwa hawajakubaliwa ombi lao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0564afe286bb187f29524b0e5588139e.jpeg

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi