loader
Vihiga bingwa Kombe la Samia

Vihiga bingwa Kombe la Samia

WENYEJI wa mashindano ya kufuzu fainali za Afrika za Wanawake, Vihiga Queens imetwaa ubingwa wa Kombe la Samia Cecafa kwa kuifunga Commercial Bank of Ethiopia (CBE) kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Kasarani, Nairobi Kenya.

CBE ambao walikuwa hawajafungwa mpaka walipofuzu fainali waliifunga Lady Doves kwa penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 120 kwa sare ya 1-1 na Vihiga Queens waliifunga Simba Queens kwa mabao 2-1 katika mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Simba Queens ya Tanzania bara imeshika nafasi ya nne baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Lady Doves ya Uganda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa mapema mchana.

Kwa matokeo hayo bingwa Vihiga Queens imeondoka na zawadi ya kombe na Dola za Marekani 30,000, CBE ikaondoka na 20,000

na Lady Doves ikaambulia 10,000 lakini pia zilikuwepo zawadi za mchezaji mmoja ambapo mfungaji bora ni Geinore Loza Abera wa CBE aliyepachika mabao 13.

Katibu Mkuu wa FIFA Fatma Samoura, ndiye alikuwa mgeni wa heshima katika fainali hizo akifuatana na ofisa wa soka la wanawake wa FIFA, Sarai Bareman.

Vihiga Queens atawakilisha Cecafa katika fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika Misri ikiungana na Wadi Degla SC ya Misri ambao ndio wenyeji, Mamelodi Sundowns Ladies FC (Afrika Kusini /COSAFA).

Nyingine ni AS FAR (Morocco/UNAF), AS Mande (Mali/WAFU I), Hasaacas Ladies FC (Ghana/WAFU II), Rivers Angels FC (Nigeria/WAFU II) na mshindi wa kanda ya UNIFFAC ambao bado hawajamaliza.

Mashindano haya ya kwanza yalianza Agosti 28 yakishirikisha timu nane ambazo ni PVP ya Burundi, FAD ya Djibouti, Lady Doves ya Uganda, Simba Queens ya Tanzania, New Generation ya Zanzibar, Yei Joint Stars ya Sudan Kusini, CBE ya Ethiopia na bingwa Vihiga Queens ya Kenya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/93d954aaf0959371927db3927022dfc0.jpeg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi