loader
BIASHARA YAIKAMIA DIKHIL

BIASHARA YAIKAMIA DIKHIL

KOCHA Mkuu wa Biashara United, Patrick Odhiambo, amesema kikosi chake kipo tayari kuwakabili Dikhil FC ya Djibouti, kwenye uwanja wa Stade du Ville leo.

Biashara iliyoanzishwa mwaka 1990, imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kumaliza ya nne kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Akizungumza na gazeti hili jana, Odhiambo alisema, amemaliza kuwaandaa vijana wake kilichobaki ni kuona kama wataenda kukifanyia kazi kile walichojifunza katika uwanja wa mazoezi.

“Najua utakuwa mchezo mgumu kwetu kikosi changu hakina uzoefu wa kutosha na michuano mikubwa ya Afrika, lakini pia tunaanzia ugenini jambo linalohitaji umakini sana.

“Tumepata nafasi ya kuangalia baadhi ya michezo ya wapinzani wetu wana timu nzuri lakini kwa maandalizi tuliyofanya naamini tunaenda kupata matokeo mazuri,” alisema Odhiambo.

Alisema kuwa wachezaji wote waliosafiri wako katika hali nzuri hakuna mwenye majeruhi hivyo kilichobaki watanzania waishio Djibouti, wasapoti timu kwani itakuwa pale ni kuipeperusha bendera ya taifa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/068d2ad3031905c1424e3013b9d493c8.jpeg

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi