loader
Dstv Habarileo  Mobile
Boris Johnson aanza kutimua mawaziri

Boris Johnson aanza kutimua mawaziri

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson leo ameanza kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa taifa hilo baada ya kupata nafuu ya janga la Corona.

Katika kauli yake iliyochapishwa na mtandao wa ‘Reuters’ msemaji wa Boris, Max Blain amesema “Tunajua wananchi wanataka tuwape vipaumbele vyao, hii ndio sababu Waziri Mkuu anataka kuhakikisha watu sahihi wapo kwenye nafasi.”

Waziri wa Elimu, Gavin Williamson amekuwa wa kwanza kuondolewa katika  nafasi hiyo na Waziri wa Sheria, Robert Buckland naye ameondolewa pia.

Taarifa zinaeleza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Dominic Raab huenda naye akaondolewa katika nafasi hiyo. Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e196aeb2563e6789885d8174e2e0ba9b.jpg

Aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni nchini Marekani, ...

foto
Mwandishi: DOWNING STREET, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi