loader
Dstv Habarileo  Mobile
RC Malima aliwekea mikatati zao la mkonge

RC Malima aliwekea mikatati zao la mkonge

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amesema miongoni mwa mikakati ya kufufua zao la Mkonge ni kuhakikisha malighafi za zao hilo zinasafirishwa kwa kutumia bandari ya mkoani humo.

Kauli hiyo ameitoa leo alipofanya ziara ya kukagua ufanisi wa Bandari ya Tanga katika kuhudumia shehena ya mizigo ya singa za katani kwenda nje ya nchi.

Amesema kuwa malengo ya Mkoa huo ni kuhakikisha Mkonge wote unaozalishwa mkoani humo usafirishwe kwa kutumia bandari hiyo tu.

"Niwatakae Mamlaka ya Bandari nendeni mkashughulikie changamoto ambazo zinasababisha wafanyabiashara kuacha kutumia bandari hii na badala yake kutumia bandari nyingine za jirani" amesema RC Malima.

Aidha amesema kuwa nia ya Mkoa huo ni kuona namna ambavyo zao hilo linaweza kuleta mafanikio kwa kasi kupitia nyanja zote za kiuchumi.

Naye Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Donald Ngaire amesema kuwa ili kuongeza ufanisi wa bandari hiyo watakutana na wafanyabiashara ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi

foto
Mwandishi: Na Amina Omari, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi