loader
Dstv Habarileo  Mobile
Polisi Morogoro wamsaka mtuhumiwa wa mauaji ya watu watatu

Polisi Morogoro wamsaka mtuhumiwa wa mauaji ya watu watatu

JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamsaka mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Abdul Abdallah mkazi wa Manispaa ya Morogoro, kwa tuhuma za kuwafungia watu wanne ndani, kumwaga mafuta ya petroli kisha kuchoma moto nyumba, mkasa uliosababisha vifo vya watu watatu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro , Fortunatus Muslimu alisema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari  juu ya  opereshani  iliyofanyika ya kwa muda wa siku 20 kuanzia Augosti 28,  hadi Septemba 16, mwaka huu ya kupambana na uhalifu kwenye Wilaya zote za Mkoa huo.

Alisema ,mtuhumiwa huyo ambaye ni mkwe wa Salima Abdallah (56) mkulima na mkazi wa Ngajima , alichoma moto nyumba ya mkwewe iliyojengwa kwa miti na kuenzekwa kwa nyasi ambapo alifunga mlango na kisha kumwagia mafuta ya petroli na kusababisha majeruhi kwa watu wanne.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Jasmini Mpoyoka (23), Shadia Matenganya (23), Sheila Mpoyoka (17), na Sofia Katikula (23)  wote wakazi wa Ngajima, Kata ya Mipepa, Tarafa ya Lupiro, wilayani Ulanga.

Kamanda Muslimu alisema sababu zilizomfanya mtuhumiwa huyo kufanya kitendo hicho ni kutokana na mgogoro wa kifamilia  baada ya mke wake, Jasmin  Mpoyoka kukataa kurudi nyumbani , ndipo alipoamua kumtafuta nyumbani kwao  na kumbembeleza kurudi nyumbani.

Muslimu alisema jitihada za kumtafuta mtuhumiwa bado zinaendelea kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama  wilaya ya Ulanga  na kufumia fursa hiyo kuomba ushirikiano  kutoka kwa wananchi  ili mtuhimiwa atiwe mbaroni.

foto
Mwandishi: Na John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi