loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ujenzi VETA kila halmashauri  nchini waanza kutekelezwa

Ujenzi VETA kila halmashauri nchini waanza kutekelezwa

S ERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango wa kuwafanya Watanzania wote kuwa na utaalamu wa fani mbalimbali kuiwezesha nchi kuwa na hazina kubwa ya watu wenye ujuzi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema hayo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika wilaya hiyo.

Alisema chuo hicho ni moja ya vyuo 29 vinavyojengwa kwenye halmashauri mbalimbali nchini.

Majaliwa alisema kwa awamu ya kwanza, jumla ya vyuo 29 vya Veta vinajengwa nchini na mpango wa serikali ni kuhakikisha vinajengwa kwenye kila halmashauri nchini.

Alisema pamoja na kumaliza elimu mbalimbali, lakini serikali inakusudia kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na ujuzi maalumu ambao atautumia kwa kazi na shughuli zitakazojitokeza na hivyo kuondoa uhaba wa wataalamu wa fani mbalimbali.

Majaliwa alisema uwekaji wa jiwe la msingi katika chuo hicho ni chachu ya kuhakikisha serikali inatenga fedha na vyuo hivyo vinaendelea kujengwa nchi nzima.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu wakati wa uwekaji huo wa jiwe la msingi, Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Pancras Bujuru, alisema ujenzi wa chuo hicho ni sehemu ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa vyuo 29 katika halmashauri zote nchini.

Bujuru alisema kuwa ujenzi wa Chuo cha Veta Buhigwe umegharimu Sh bilioni 2.4 ikiwa ni sehemu ya Sh bilioni 48.6 zitakazotumika kwa vyuo hivyo kwa awamu ya kwanza.

“Matarajio yetu ni kuona idadi kubwa ya Watanzania wanakuwa na elimu maalumu ya utaalamu ambapo kila chuo katika vyuo 29 vinavyojengwa kinatarajia kuchukua wanafunzi 260 ambao watasomea fani zaidi ya sita zinazotolewa kwenye vyuo hivyo,” alisema.

Naibu Waziri , Ofisi ya Rais-Tamisemi, David Silinde alisema serikali imedhamiria kuboresha utoaji elimu nchini kwa kuongeza fedha kwenye nyanja mbalimbali za elimu

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi