loader
Dstv Habarileo  Mobile
‘Muda wa kushughulikia  kero za wananchi ni sasa’

‘Muda wa kushughulikia kero za wananchi ni sasa’

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye, amewataka wanasiasa wakiwemo wabunge na madiwani wanaohangaika kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao 2025 kuacha mara moja na badala yake wajikite katika kushughulikia kero za wananchi.

Kiboye alitoa tahadhari hiyo wakati akifungua kikao cha Baraza la Vijana Mkoa wa Mara na kufafanua kwamba katika mkoa huo wa Kanda ya Ziwa kumeibuka makundi ya wanasiasa yameanza kujiandaa na uchaguzi ujao, jambo ambalo ni kinyume na taratibu, kanuni na miongozo ya chama hicho kikongwe kinachotawala nchi.

Aliwataka wabunge na madiwani kuacha kuhangaika na uchaguzi huo na badala yake wafanye kazi waliyoiomba ya kuwatumikia wananchi hadi muda utakapofika.

Alisema pamoja na kuwapo kwa haki ya kila mwana CCM kugombea nafasi yoyote, wakati haujafika na kwamba kipindi cha sasa ni kuhakikisha kwamba wanasimamia serikali kutekeleza wajibu wake kwenye utekelezaji wa Ilani ya CCM iliyowawezesha kushika dola.

“Ndugu zangu hivi sasa tunatakiwa kutekeleza maagizo ya Rais wetu ya kutaka viongozi kuhangaika na utatuzi wa kero za wananchi kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya na mkoa.

Sasa mnaohangaika na kupanga safu badala ya maelekezo ya mkuu wa nchi tuwaelewaje?” Alihoji.

Alisema wananchi wana kero nyingi zinazohitaji kutatuliwa, zikiwemo za migogoro ya ardhi, barabara, maji, huduma za afya na nyinginezo na kwamba hayo ndiyo mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na viongozi hao sasa na siyo vinginevyo.

Kiboye alisema kutokana na hali hiyo, kamati ya siasa ya mkoa imepanga kufanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ili kuangalia namna viongozi wan

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Mara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi