loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia kushiriki mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Marekani

Rais Samia kushiriki mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Marekani

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakao fanyika Jijini New York, Marekani ambapo pia atahutubia Baraza hilo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Rais Samia ataondoka nchini Septemba 18. Rais Samia anatarajiwa kuhutubia Baraza hilo Septemba 23.  Hii ni safari ya kwanza ya Rais Samia kufanya safari za mbali ya Bara la Afrika tangu aingie madarakani Machi mwaka huu.

“Pamoja na Mkutano huo, Mhe. Rais Samia pia atahudhuria mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs),” imesema taarifa ya Ikulu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Jaffar Haniu amesema Rais Samia atakutana na Wakuu wa Nchi nyingine na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania nan chi na taasisi zao.

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi