loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mbaroni kwa kuvujisha mitihani

Mbaroni kwa kuvujisha mitihani

WATU sita wakiwemo watumishi wa serikali wilayani Mvomero wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na njama za kuvujisha mtihani wa taifa wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kambara iliyopo wilayani humo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu amesema watu hao sita, baadhi yao ni walimu wa shule za msingi na wengine sekondari katika wilaya ya Mvomero wanaendelea kushikiliwa kwa mahojiano wakituhumiwa kuhusika na njama za kuvujisha mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 8 na Septemba 9 mwaka huu.

Aliwataja wanaoshikiliwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambala, Juliana Nyumayo (40), Msimamizi Mkuu wa Mtihani katika shule hiyo, Antonia Pastory (32) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Doma na mkazi wa Doma wilayani Mvomero pamoja na msimamzi wa mtihani wa mkondo C, Francis Kondo (46) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Kinda, wilayani Mvomero.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi