loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia ataka ufanisi Wizara ya Habari

Rais Samia ataka ufanisi Wizara ya Habari

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais Samia Suluhu ameamua kuihamisha Idara ya Habari - Maelezo kwenda Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari sababu kubwa ni kuongeza ufanisi.

Wiki iliyopita Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, ambapo ameihamishia Idara ya Habari katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

Akizungumza leo na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo, Msigwa alisema “Rais Samia ameihamisha Idara ya Habari - Maelezo kwenda Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari sababu kubwa ni kuleta ufanisi zaidi na kuipeleka Idara katika eneo ambalo utendaji wake wa kazi unaendana na shughuli za wizara husika.

Aidha baada ya Wizara hiyo kuhamishwa Rais Samia alitengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wake, Dk Faustine Ndugulile na kuteuliwa Dk Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi