loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali kuuza chakula nchi zenye upungufu

Serikali kuuza chakula nchi zenye upungufu

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali inaangalia namna ya kufanya majadiliano na baadhi ya nchi kuona namna watakavyoweza kuuza chakula kwenye nchi zenye upunugufu wa chakula.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi na wananchi kwa njia ya simu katika ukumbi wa Habari Maelezo ulipo jijini Dodoma leo.

“Nchi yetu ina ziada ya chakula zaidi ya tani 3,600,000 ambazo wakulima wetu wamezalisha na wanatafuta masoko, kwenye vikao hivyo watajadili namna gani nchi zitabadilishana vyakula na Tanzania ipate fursa ya kuuza chakula sehemu zenye upungufu.”

 

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi