loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chama skauti wa kike chapewa changamoto udhalilishaji

Chama skauti wa kike chapewa changamoto udhalilishaji

NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassani Juma amekitaka chama cha skauti wa kike Tanzania kilete mabadiliko kwa watoto wa kike na kupambana na udhalilishaji wa kijinsia.

Mgeni aliyasema hayo jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro alipozungumza na viongozi wa skauti wa kike kutoka katika mikoa 20 ya Tanzania bara na Zanzibar.

Alisema unyanyasaji wa kijinsia umekuwa kero katika jamii hivyo chama hicho kina wajibu wa kuhakikisha kinaleta mabadiliko ya kweli kwa wanachama wake.

“Kwa sasa changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu ni kubwa sana na suala hilo limekuwa likileta maudhi na kadhia kwa watu wengine jambo ambalo linapaswa kukemewa na watu wa kada zote wakiongozwa na chama hichi"alisema Mgeni.

Aliwataka watoto wa kike wajiandae na kujijenga katika misingi ya kuwa viongozi bora katika jamii na kuwa mstari wa mbele kujitolea katika shughuli za maendeleo.

"Jijengeeni msingi ya kujiamini na kuwa viongozi bora na mnaokubalika katika jamii ili muondoe dhana ya wanawake hawawezi, shirikini katika shughuli mbalimbali za jamii kwa kujitolea kwa moyo mtaona faida yake hapo baadaye"alisema Mgeni.

Kamishna Mkuu wa chama hicho, Symphorosa Hangi alisema wamejipanga kuleta mabadiliko kwa watoto wa kike kwa kuwajengea uwezo wa kujiamini.

Kamishna wa Skauti wa kike Mkoa wa Pwani, Martha Mshiu alisema wamejiwekea mkakati wa kutoa elimu kwa mtoto wa kike ili kusaidia kukabili changamoto za ukatili wa kijinsia.

foto
Mwandishi: Na Upendo Mosha, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi