loader
Dstv Habarileo  Mobile
SMZ yaridhishwa na mila, utamaduni

SMZ yaridhishwa na mila, utamaduni

SERIKALI ya Zanzibar imesema inaridhishwa na harakati za kukuza mila, utamaduni na sanaa.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Fatma Hamad katika Maulid ya Jumuiya ya Bora Utu Kuliko Kitu ya  Tumbatu Jongowe, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema juhudi hizo zinafanywa na wizara na kuungwa mkono na vijana na kwamba wapo tayari kusaidia kwa namna yoyote.

"Tunafurahi mila na utamaduni mmekuwa mkiudumisha katika masuala ya dini na mambo ambayo yamekuwa yakitoweka na kupigwa vita dunia mzima," alisema.

Alisema dunia hivi sasa imegeuka na kufanya mambo yote ya mila, sanaa na utamaduni yanaonekana sio muhimu kutokana na utandawazi.

"Watu wamekuza zaidi mambo ya nje kwa sababu ya kuongezeka kwa televisheni ambazo zinawapa mambo mbalimbali ya nje na kufua na kuacha ya nchini kwao,", alisema Mnemo.

Akizingumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa na Utamaduni (BASFU) Dk. Omar Abdallah alisema baraza lao limekuwa na jukumu la kuhamasisha na kuwaendeleza vijana katika kulinda mila, silka, na utamaduni wa Mzanzibar.

Mapema wakati akisoma risala ya jumuiya hiyo, Adam Jecha Mngwali alisema Jumuia yao imekuwa ikitoa zaka na sadaka lakini kutokana na kipato chao kuwa kidogo kinakuwa hakitoshi.

Alisema mpaka sasa jumuiya ina wanachama 30 na inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vifaa vya kutendea kazi, ukosefu wa jengo la kudumu la ofisi .

Jumuiya pia inajishulisha na kilimo cha mboga mboga kwa ajili ya kujiongezea kipato.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d2af9bf2e34880d48719f1063ea96a1f.jpg

MSANII wa Bongo Movie  ambaye pia ni ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi