loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanesco yatenga bilioni 1 kununua mitambo ya umeme Geita

Tanesco yatenga bilioni 1 kununua mitambo ya umeme Geita

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limetenga Sh bilioni 1.3 katika bajeti yake ya mwaka huu wa fedha kununua vifaa na mitambo kwenye kituo cha mfano cha uchenjuaji madini cha Katente wilayani Geita mkoani hapa.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Stamico, Venance Mwasse wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya kituo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipofanya ziara yake kukagua miradi ya maendeleo ya sekta hizo.

Alisema maboresho yanafanyika ili kukidhi huduma ya uchenjuaji ambapo kituo (bila mitambo) kiligharamu Sh bilioni 1.7, ikiwa ni sehemu ya  mradi wa kitaifa wa uanzishwaji wa vituo vya mfano vya uchenjuaji madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

“Vingine ikiwa ni Lwamugasa-Geita na Itumbi-Chunya. Gharama za jumla za ujenzi wa vituo hivyo vya mfano  uligharimu kiasi cha Sh billioni 4.3 ambazo zilijenga vituo vya Katente-Bukombe, Lwamugasa-Geita na Itumbi-Chunya mkoani Mbeya,” alisema.

Alisema toka kituo cha Katente kuzunduliwa mwaka jana hadi Agosti 2021, kimeweza kuchakata jumla ya tani zipatazo 858.6 za madini kutoka kwa wachimbaji wadogo, kati yake ziliweza kuzalisha dhahabu kiasi cha gramu 5,874.40 yenye thamani ya Sh milioni 712.9 .

Kuanzia Aprili 26 mwaka 2020 hadi Agosti 2021 jumla ya wachimbaji wadogo 464 wametembelea kituo hicho na kupata elimu huku jumla ya awamu 37 za uchenjuaji kutoka kwa wateja wa nje ya kituo zimefanyika na kuzalisha gramu 9,822.93 za dhahabu yenye thamani ya Sh bilioni1.2

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Self Hamis alieleza kuridhishwa na mwenendo wa usimamizi na uendeshaji wa kituo na kuwataka wasimamizi kuendelea kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

foto
Mwandishi: Na Yohana Shida, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi