loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waliomdhiti Hamza watuzwa 500,000/-

Waliomdhiti Hamza watuzwa 500,000/-

POLISI 11 walioshiriki kumdhibiti kijana aliyeua polisi watatu na askari wa kampuni ya ulinzi ya SGA, Hamza Mohamed wametunukiwa vyeti na fedha Sh 500,000/- kila mmoja.

Kamanda wa jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema jana kuwa wametoa zawadi hizo kwa kuwa walifanya kitendo cha kijasiri katika tukio la Agosti 25 mwaka huu.

Katika tukio hilo kijana huyo aliyedaiwa kuwa mkazi wa eneo la Fire, Upanga jijini Dar es Salaam alishambulia askari kwa risasi jirani na daraja la Selander na Ubalozi wa Ufaransa.

Taarifa za awali za polisi zileleza kuwa, siku ya tukio kijana hiyo aliyedaiwa kuwa mfanyabiashara wa madini aliua polisi watatu kwa risasi na akachukua silaha zao na kuendelea kushambulia.

Mwanzoni mwa mwezi huu Jeshi la Polisi lilitangaza kuwa kijana huyo alikuwa gaidi, aliishi kwa siri na alikuwa akijifunza vitendo hivyo kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Kamanda Muliro, askari wote walifanya kazi nzuri kupambana na kijana huyo lakini jeshi limeona liwazawadie 11 kwa kuwa walijituma zaidi.

“Kitendo walichokifanya ni cha kijasiri mno, mtu ana silaha na unajua ukisogea unaweza kufa lakini hawakuogopa hilo walipambana hadi kumdhibiti, kwetu hii ndiyo kazi unajitolea kupoteza maisha kwa ajili ya watu wengine”alisema.

Kamanda Muliro alisema Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na uhalifu kwa kuwadhibiti wote wenye nia ovu na akaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Polisi ili wahalifu wakamatwe.

Aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa, mwananchi yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa mtu/watu wanaotumia silaha kufanya uhalifu atapata zawadi ya Sh milioni mbili.

Alisema polisi wataficha siri za yeyote atakayetoa taarifa na pia zawadi ya fedha itatolewa bila kutangazwa.

Aidha mmoja wa askari aliyezawadia kutokana na tukio hilo, Mashaka Masime alisema alijitolea kupambana na Hamza kwa kuwa aliapa kulitumikia taifa na wananchi hadi walipomshinda mhalifu.

Aliwaomba polisi wasirudi nyuma au kutishwa na kitendo cha wenzao kupoteza maisha bali iwe chachu kwao ya kuendeleza mapambano dhidi ya wahalif

foto
Mwandishi: Oscar Job na Bernadetha Mushi (TUDARCo)

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi