loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa ashtukia ufisadi  ofisi ya Tanesco

Majaliwa ashtukia ufisadi ofisi ya Tanesco

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofi si ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.

Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa Majaliwa alitoa uamuzi huo jana akiwa katika katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye mkoa huo.

“Nikiweka jiwe la msingi nitakuwa nimehalalisha majengo mengine yajengwe kwa gharama hii. Siwezi kuweka jiwe la msingi, gharama zilizotumika ni kubwa kuliko majengo yaliyopo.

Simamieni ujenzi wa majengo yenu na mjenge kwa kutumia mfumo wa force account,”alisema.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa ujenzi huo umegharimu Sh milioni 483.42 na kwamba kibanda cha mlinzi kimegharimu shilingi milioni 7.03, uzio Sh milioni 94.2, jengo la ofisi Sh milioni 253.8 na stoo Sh milioni 51.55.

“Nini kilisababisha hadi kibanda kidogo cha mlinzi kikajengwa kwa shilingi milioni saba? Kina matofali mangapi kama sio ulaji nini? hii si sahihi sijaweka jiwe la msingi wala kufungua na kile kibao kilichoandikwa jina langu kiondolewe.

Serikali ipo makini katika usimamizi wa miradi na haya ni maelekezo ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,”alisema Majaliwa.

Alisema serikali inajenga majengo makubwa ya vituo vya afya vyenye jengo la mapokezi ya wagonjwa, maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya mama na mtoto, nyumba ya daktari, chumba cha kuhifadhia maiti, kichomea taka na korido kwa gharama ya Sh milioni 500.

Majaliwa aliuagiza uongozi wa Tanesco uhakikishe gharama za miradi yake zinalingana na aina na idadi ya majengo.

Meneja Mwandamizi Usambazi wa Tanesco makao makuu, Nathanasias Nangali alisema mradi huo ulianza Septemba 11, 2018 na kukamilika Februari 08 mwaka jana kwa gharama za Sh 483,422,328.02.

Nangali alisema shirika hilo limeendelea kutenga fedha kwa awamu kila mwaka ili kutekeleza miradi kama hiyo na katika mwaka huu wa fedha linajenga ofisi za wilaya za Buhigwe-Kigoma, RuangwaLindi, Urambo-Tabora, Gairo na Malinyi-Morogoro, Nanyumbu na TandahimbaMtwara, Kilolo-Iringa, Rorya na Serengeti-Mara, LaelaRukwa na Meatu-Simiyu.

“TANESCO imeendelea kutumia wataalamu wake katika kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa ofisi zake za mikoa, wilaya na vituo vya kupoza na kusambaza umeme,”alisema.

Akizungumzia huduma ya umeme inayotolewa katika wilaya hiyo amesema kati ya vijiji 99 vya wilaya hiyo vijiji 70 vinaumeme na vijiji 29 vilivyosalia vitapata huduma hiyo kupitia mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili unaoendelea kutekelezwa.

Awali, Majaliwa alitembelea na kukagua kiwanda cha kuchenjua madini ya bati (TIN) cha kampuni ya African Top Minerals kilichopo wilayani Kyerwa.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hassan Ibar alisema mradi huo uliogharimu shilingi bilioni nne una lengo la kuboresha sekta ya madini wilayani humo na Tanzania kwa kuongeza thamani ya madini hayo kwenye soko la du

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi