loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kocha Biashara aichekelea Simba

Kocha Biashara aichekelea Simba

KOCHA Mkuu wa Biashara United, Patrick Okumu amesema kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza na mabingwa watetezi Simba, ni kipimo kizuri kwa timu yake kuelekea mchezo wao wa raundi ya kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

Septemba 27 Biashara United itaikaribisha Simba katika Uwanja wa Karume Mara kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Okumu alisema anajua ubora wa Simba na ni miongoni mwa timu bora Afrika, hivyo mbali yakuwa ni mechi watakayohitaji kupata ushindi, lakini ni kipimo kizuri kwao kuelekea mchezo wao unaofuata wa kimataifa dhidi ya Al Ahli ya Libya.

“Najua tunakwenda kucheza na bingwa mtetezi wa Tanzania haitakuwa mechi nyepesi kwa timu zote, lakini kwetu Biashara itakuwa ni maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu wa hatua ya kwanza wa michuano hiyo,” alisema Okumu.

Kocha huyo alisema amefurahi kuanza msimu na bingwa mtetezi Simba sababu itamsaidia kujua uimara wa kikosi chake.

Alisema tangu kumalizika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Dikhil ya Djibouti wanaendelea na maandalizi kuelekea mechi za ligi pamoja na mchezo huo wa kimataifa utakaochezwa mwezi ujao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b43b744c871ecb3ff5f4e1782ee357e8.JPG

TIMU ya Taifa ya Soka la Watu wenye ...

foto
Mwandishi: MOHAMED AKIDA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi