loader
Dstv Habarileo  Mobile
Acheni siasa kwenye Corona

Acheni siasa kwenye Corona

MKUU  wa mkoa wa Tanga, Adam Malima, amewataka watàalamu wa afya kuacha kuingiza siasa katika kupeleka elimu ya kuhamasisha chanjo ya ugonjwa wa Covid 19  kwa wananchi.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa kikao cha tathimini ya utoaji wa chanjo Corona kwa wananchi wa mkoani huo.

Amewataka wataalamu hao kujikita katika kutoa elimu ili kuweza kuongeza uwelewa kwa wananchi na hivyo kuondoa dhana mbaya iliyoko katika jamii.

"Wataalamu wa afya kama mmeweza kuhamasisha wazazi kuna umuhimu wa kuchanja watoto wachanga basi nendeni mkahamasishe watu umuhimu wa chanjo ili kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona" amesema Malima.

Aidha aliwaasa wanasiasa na viongozi wa dini kuendelea kutumia majukwaa yao kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuona manufaa ya kuchanja ili kuendelea kujilinda na maambukizi mapya.

Hata hivyo akitoa takwimu za chanjo kwa mkoa huo Mganga Mkuu wa mkoa Dk Jonathan Budenu,  alisema kuwa lengo ni kuchanja walengwa 139, 000 lakini wameweza kufikia watu 10,939 sawa na asilimia 31

Amesema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutoa chanjo katika maeneo yenye mikusanyiko kama shuleni, sokoni, kwenye misikiti , makanisa pamoja na vyombo vya usafiri

foto
Mwandishi: Amina Omari, Tanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi