loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rasilimali za nchi zitainua uchumi- Majaliwa

Rasilimali za nchi zitainua uchumi- Majaliwa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu, imedhamiria kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinachangia katika kuinua uchumi wa Watanzania.  

" Rais Samia, anawaahidi kuendelea kuchukua hatua madhubuti katika kulinda na kuendeleza rasilimali hizi ili ziweze kuwanufaisha na kuwaletea maendeleo watanzania wote, tuendelee kuunga mkono."

Waziri Mkuu ameseyasema hayo leo Jumatano, Septemba 22, 2021 baada ya kuzindua Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini mkoani Geita.

Amesema maonesho hayo yamekuwa na manufaa makubwa katika kuhamasisha wananchi kujihusisha na shughuli za madini.

 Amesema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni na taratibu zinazosimamia uchimbaji na biashara ya madini kwa lengo la kuwezesha wananchi na wadau mbalimbali kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini na kuongeza uwekezaji.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi