loader
Dstv Habarileo  Mobile
Zingatieni sheria, kanuni na miongozo- Majaliwa

Zingatieni sheria, kanuni na miongozo- Majaliwa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wadau wa sekta ya madini nchini kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayosimamia sekta hiyo ili kuondoa usumbufu na kurahisisha utendaji wa shughuli zao na Serikali kwa manufaa ya pande zote. 

Amesema sekta ya madini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini.

“Matarajio ya Serikali ni kuongeza zaidi mchango huo kupitia shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji madini, usanifu madini na utoaji wa huduma katika shuguli za madini.”

“Lengo la Serikali ni kufungamanisha ustawi wa sekta ya madini kwa kuwezesha wananchi na wadau mbalimbali kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini na kuongeza uwekezaji ili kukuza sekta nyingine za kiuchumi na huduma zikiwemo viwanda, ujenzi, usafirishaji, mawasiliano na nishati.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi