loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk Mabula asitisha huduma za kampuni tatu

Dk Mabula asitisha huduma za kampuni tatu

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amesitisha huduma za kampuni tatu zilizokuwa zinarasimisha makazi katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kwa kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati.

Dk Mabula amefukia hatua hiyo wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo akiwa katika muendelezo wa ziara yake.

Ameagiza Ofisi ya Ardhi ya Mkoa kukaa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bahi iundwe na timu ya Mkoa ije hapa kwa gharama ya Mkurugenzi ili kukamilisha upimaji.

Aidha,  Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Thadei Kabonge amesema Kumeibuka tabia kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutojitokeza kuchukua hati zao za umiliki wa ardhi kwa wakati kwa kigezo cha kukwepa kulipa kodi ya pango ardhi kitu ambacho kwa sasa Bunge limeipatia muarubaini tabia hii.

Kabonge ameongeza kuwa mwaka jana Bunge lilipitisha sheria kwamba ardhi ikishapimwa na ikapita miezi mitatu na mmiliki hajajitokeza kuja kumilikishwa itahesabika tayari ushamilikishwa na itaanza kuhesabiwa kodi ya ardhi.

Aidha, Kabonge wametakiwa wananchi kujitokeza ili kumilikishwa Ardhi kisheria kwa kukwa kutomilikishwa ardhi sio kigezo cha kukwepa kulipa kodi ya ardhi hata kama ardhi hiyo itakuja kumikishwa baada ya miaka kupita.

Kamishna Kabonge amebainisha kuwa ofisi yake ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma ina viwanja zaidi ya 2,550 ambavyo vimepimwa tayari lakini wananchi hawataki kumilikishwa.

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi