loader
Dstv Habarileo  Mobile
MWANDISHI  ITV/RADIO ONE AFARIKI, MWINGINE AJERUHIWA

MWANDISHI ITV/RADIO ONE AFARIKI, MWINGINE AJERUHIWA

MWANDISHI wa Habari wa ITV na Radio One mkoani Songwe Gabriel Kandonga, amefariki dunia kwa ajali ya gari.

 

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Septemba 24, 2021, wakati akitokea nyumbani kwake Mpemba kuelekea wilayani Songwe katika majukumu yake ya kila siku.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba, amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwandishi huyo na kusema ajali hiyo imetokea katika eneo la shule ya Sekondari Mlowo ambapo alikuwa anajaribu kulipita lori na hatimaye kulivaa fuso kwa upande wa nyuma.

Mgumba amesema katika ajali hiyo Kandonga alikuwa na Mwandishi mwenzake wa Clouds TV Haika Sanga ambae anaendelea na matibabu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi