loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia: Tanzania ni ile ile

Rais Samia: Tanzania ni ile ile

RAIS Samia Suluhu, ameihakikishia dunia kuwa Tanzania ni ile ile yenye amani na ushirikiano kwa nchi zote.

Kauli hiyo ameitoa leo kupitia mtandao wake wa Twitter mara baada ya usiku wa kuamkia leo Septemba 24, 2021, kuhutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

"Nimehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nimeihakikishia dunia kuwa Tanzania ni ile ile yenye amani na ushirikiano na nchi zote, nimeeleza imani yangu kuwa changamoto za dunia tunaweza kuzikabili kwa pamoja ikiwemo janga la Uviko-19," amesema Rais Samia.

Aidha katika hotuba yake ya jana usiku, Rais Samia ameuomba Umoja wa Mataifa kuondoa hati miliki kwenye uzalishaji wa chanjo ya Covid - 19 ili mataifa mengi yaweze kuizalisha na kuitoa kwa wananchi wake la sivyo itakua ngumu kufikia malengo yaliyowekwa na Shirika la Afya Dunia (WHO)

Amesema kasi ya utengenezaji na usambazaji wa chanjo ya Covid -19 imekuwa ndogo ikilinganishwa na kasi ya usambaaji wa ugonjwa huo .

“Kwa hali ilivyo sasa ni wazi kwamba itakuwa ngumu sana kufikia malengo yaliyowekwa na Shirika la Afya Duniani la kuchanja angalau asilimia 40 ya watu katika kila nchi hadi kufikia mwisho wa mwaka 2021 na asilimilimia 70 hadi kufikia katikati ya mwaka 2022.

“Hakuna aliye salama hadi wote tuwe salama, ni muhimu nchi zenye chanjo zisaidie nchi zisizo na chanjo ili kukabiliana na janga hili la Uviko-19,” amesisitiza Rais Samia.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi