loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ushahidi kesi ndogo ya Mbowe wafungwa, sasa kuanza kujitetea

Ushahidi kesi ndogo ya Mbowe wafungwa, sasa kuanza kujitetea

UPANDE wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ushahidi umefungwa  baada ya kuwaita mashahidi watatu.

Wamefunga ushahidi wao leo Ijumaa Septemba 24, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo sasa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ndogo ambaye ni mshtakiwa wa pili Adam Hassan anatarajia kuanza kujitetea.

Kesi hiyo ndogo inahusu uhali wa uchukuaji wa maelezo yake polisi baada ya kukamatwa.

Mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokelewe Mahakamani kama kielelezo cha usahidi wa upande wa mashtaka wakidai kuwa kabla na wakati wa kuyatoa maelezo hayo mshtakiwa huyo aliteswa.

Walidai pia maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda unaoruhusiwa kisheria.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi