loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tamisemi yatoa wiki 22 Halmashauri 22

Tamisemi yatoa wiki 22 Halmashauri 22

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Profesa Riziki Shemdoe amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri 22 ambao hawajaingiza taarifa zao za hesabu za mwisho  kwenye mfumo wa Serikali wa uandaaji wa hesabu kufanya hivyo ndani ya siku mbili.

Amezitaja baadhi ya Halmshauri hizo ni Dar es Salaam jiji (Jiji la zamani), Mvomero DC, Chalinze DC, Madaba DC, Shinyanga DC, Muheza DC, Kishapu DC, Kahama MC, Lushoto DC, Bahi DC, Newala DC, Newala TC, Kibaha DC, Songea DC, Itilima DC, Manyoni DC, Songwe DC,  Bumbuli DC, Kilindi DC,  Msalala DC,

Amesema ifikapo Septemba 30 mwaka huu ambao bado watakuwa hawajatekeleza agizo hilo wajiandae kwa kupata hati chafu au zenye mashaka.

Hayo ameyasema jijini hapa leo Septemba 24, 2021 wakati wa kikao kazi cha siku mbili na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi