loader
KANU kumtangaza mgombea urais wiki hii

KANU kumtangaza mgombea urais wiki hii

UONGOZI wa Chama cha Kenya African National Union (KANU), umesema chama hicho kitasimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao mwakani na atatangazwa wiki hii.

Katika mkutano na wajumbe uliofanyika Mombasa wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Kanu, Nick Salat, alisema watamtambulisha mgombea wao wa urais katika Mkutano Mkuu ujao wa mwaka utakaofanyika Alhamisi wiki hii.

"Kanu kitakuwa chama imara katika uchaguzi ujao na tuko tayari kupambana; acha turudi kwenye amani tuliyokuwa nayo enzi za utawala wetu," alisema Salat.

Chama hicho kimepangwa kukutana na wajumbe wake kutoka nchini kote katika Bomas ya Kenya keshokutwa Septemba 30, ambapo watamtangaza mgombea wao.

"Hatuhitaji kiongozi mkali; tunahitaji mtu ambaye yuko tayari kuitumikia nchi, si kwa namna wengine wanavyomuona kuwa ni mkali, bali tunataka mwenye nguvu,” alisema Salat.

Maneno ya Salat yanakuja siku chache baada ya baadhi ya wajumbe kumwidhinisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Gideon Moi, kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka ujao wakati wa mkutano huko Diani, Kaunti ya Kwale, Septemba 23.

Wajumbe hao walisema Gideon ni kiongozi mwenye busara na aliye na nafasi nzuri ya kuingiza damu safi katika utawala katika kinyang'anyiro cha kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3983f6b2aa46fdeb7c712916b2941ae8.jpg

MGANDA Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia katika ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi