loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waandishi Habari walivyo‘chambo’ kwa Covid-19

Waandishi Habari walivyo‘chambo’ kwa Covid-19

"Chanjo suluhisho la usalama wao"

KUNDI la waandishi wa habari ni miongoni mwa makundi ambayo yako hatarini kupata maambukizi yavirusivya corona hii ni kutokana na shughuli zao za kila siku kuwa na mwingiliano.

Tahadhari muhimu za kiafya zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na kuepuka mikusanyiko kwa kuweka nafasi kati ya mtu na mtu,kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono.

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za Julai 8, mwaka huu watu  408  walikuwa wamepata maambukizi ya wimbi jipya la Delta huku watu 284 wakipumulia mashine za oksijeni.

Wizara imeendelea kusisitiza watu kuendelea kuchukua tahadhari  za kujikinga na ugonjwa huo kwa kutoa mwongozo ambao unataka watu kunawa mikono kwa maji tiririka na kujitakasa mikono.

Miongozo mingine ni kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima sehemu mbalimbali ikiwemo kupunguza idadi ya abiria katika vyombo vya usafiri (level seat).

Kuvaa barakoa sehemu za mikusanyiko kama sokoni, hospitalini, taasisi za kiserikali na binafsi, vyombo vya usafiri na mikusanyiko mingine.

Lakini Je ni waandishi wangapi wanazingatia tahadhari hizo?

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa  Mwanza  Press Club,  Edwin Soko asilimia  75 ya waandishi waliopatiwa mafunzo kwa njia mbalimbali wanafata maelekezo ya kujikinga na ugonjwa wa Covid -19.

“Kuna  asilimia 25 iliyobaki hawa hawafati tahadhari huenda ni kwasababu hawajafikiwa au kupuuza,”anasema  Soko.

Jitihada zinazofanywa zinaweza kuwa msaada mkubwa kwa waandishi wa habari  kupata uelewa  na kuwaelimisha jamii.

Soko  anabainisha kuwa  kupitia club yao wanaandaa mikutano  na midahalo  kuhusu Covid-19 na chanjo.

“Katika mikutano hiyo kuna vitu tunakubaliana kama miongozo itakayosaidia waaandishi kufanyakazi zao na kujikinga ,Moja ni kuweka distance kati yake na chanzo cha habari, pili kuwa makini na kutoshirikiana vifaa.

“Tunawafundisha jinsi wanavyotakiwa kufanyakazi na namna  ya kuvaa barakoa na  kubadilia,”anafafanua.

Aidha  wanafanya uandaajiwa mikutano  ya  kimataifa  kwa kushirikiana  na Wizara  ya Afya ilikukutanisha wataalamu  wa afya mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu.

“Wataalamu wanawaeleza ili kumfanya mwandishi kuwa na weledi na  kuweza kuchuja taarifa  sahihi.

KWANINI WAANDISHI HAWAZINGATII TAHADHARI?

Mwandishi  wa  habari za afya, Harieth Makweta anasema  bado hakuna mkazo wa waandishi kuchukua tahadhari za kujingana Covid -19 licha ya kuwa wanaandika habari hizo.

Makweta  anaeleza  kuwa waandishi wa Habari wanaochukua tahadhari ni wachache na hii ni kutokana na kupuuzia  tahadhari.

“Tunaona  wengi wanaenda kucover story hawaja vaa barakoa  na wengine hawa na sanitizer lakini wanaripoti habari  za covid  wao hawachukui  tahadhari za aina yoyote  ile.

Anaongeza “Licha ya kwamba wanapewa elimu lakini bado jitihada za tahadhari hamna na tunadhani kwamba tunaweza kuwapatia watu wengine elimu na sisi hatuzingatii.

Anasema kuwa mwamko bado ni mdogo na wanapaswa kukumbushwa  wao  wenyewe  kuchukua tahadhari.

James Salvatory ni Mwandishiwa Times Fm anasema kwa kiasi kikubwa bado waandishi hawazingatii tahadhari na hii ni kutokana  na mtazamo  wa uongozi  uliopita.

“Na hii ni kwa wananchi pia wapo wanaoamini  kuwa hakuna corona licha ya serikali kuendelea kusisitiza kuwa watu  wa chukue  tahadhari,”anaeleza.

TUNAFANYA JITIHADA HIZI

Kundi la Habari ndio wanaotegemewa kufikisha elimu kwa jamii  hasa  kuhusu  janga la Covid 19.

Taasisi zinazohusika na masuala ya kihabari zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha waandishi wanapata elimu ya namna ya kujikinga.

Miongoni Mwa taasisi ambazo zinajihusisha moja kwa moja kuhakikisha waandishi wanapata uelewa ni Taasisi ya vyombo vya  Habari  kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TAN).

Kaimu  Mkurugenzi  wa MISA TAN  Andrew Marawiti anasema jitihada kubwa wanayofanya kuhakikisha waandishi wanajikinga na  virusi  vya Covid 19 nikutoa elimu kwa njia ya  mafunzo wanayoandaa.

“Tunatoa mafunzo kwa waandishi na bado tunaendelea kutoa,hivi karibuni mwezi wa saba tulifanya semina ya kuwajengea uelewa waandishi kuhusu namna ya kujikinga  na pia kuandika habari za corona.

“Na pia tuna mpango wa kuwa na mafunzo zaidi na tuko kwenye mazungumzo na wadhamini wawili na mmoja tuko katika hatua ya  maandiko ,lakini pia tunaonesha mifano  wakati  wa  mafunzo  tunafata  tahadhari  zote za kifya,”anabainisha  Marawiti.

Anashauri  kuwa ni vyema waandishi wakazingatia hatua za kujikinga pindi wanapokuwa  katika majukumu  yao.

“Bado elimu inahitajika sio  kwa  waandishi tu hata kwa wananchi walioko pembezoni hivyo waandishi wa habari wanatakiwa  kuwa mfano kwa  jamii,”anaeleza.

HabariLEO pia ilizungumza  na  Mkurugenzi  wa Baraza la Habari Tanzania(MCT),Kajubi  Mukangaja,anasema mara baada  ya  kutokea  mlipuko wa virusi  vya corona baraza hilo  liliandaa mwongozo wa kuripoti kwa weledi na usalama.

Mwangozo huo ambao ulisambazwa kwa waandishi wa habari kupitia  njia  mbalimbali pia unapatatikana katika tovuti ya MCT.

Kajubi anasema jitihada zingine walizofanya ni kuwasiliana  na  wahariri wa vyombo  vya Habari ili kuhakikisha wanawasaidia waandishi wao kujikinga wanapokuwa kazini.

“Sisi tunatoa mifano ya kujikinga kwa kuweka barakoa na vitakasa  mikono  getini ,hatufanyi mikutano wala semina kwa kukutana kila kitu tunafanyia mtandaoni kwasababu ya kujikinga.

“Hata hafla  ya utoaji  tuzo za EJAT ni wachache tu walihudhuria wengine walifatilia  kupitia mtandaoni kwa link maalum  hivyo  tunazingatia  afya za waandishi,”anafafanua  Kajubi.

Chama cha waandishiwa Habari Wanawake (TAMWA) pia wameeleza namna wanavyosaidia waandishi wa habari kujinga  na virusi  vya corona.

Mkurugenziwa TAMWA, Rose Ruben ,anaeleza kuwa  taasisi hiyo inafanya jitihada nyingi tangu kuanza kwa ugonjwa huo mmoja ikiwa ni kuzungumza na wamiliki wa vyombo  vya  Habari.

“Tumezungumza nao kuwapa vitendea kazi waandishi wanapokuwa katika majukumu yao ikiwemo  barakoa  na sanitizer.

Anasema  jitihada nyingine ni kuhakikisha waandishi wanapewa  kipaumbele  katika  kupata  chanjo ya Covid 19.

“Lakini pia tunawaelimisha kuwa baada ya kupata chanjo ni muhimu kuendelea  kuchukua tahadhari za kiafya kwani  mwandishi wa habari anaenda popote,”anabainisha.

Irene Mark ni  Mwenyekiti wa  Clabu ya  waandishi  Mkoa wa Dar es Salaam( DCPC) anabainisha kuwa utoaji wa mafunzo  ya  mara kwa mara unaongeza  jitihada za waandishiwa Habari kujikinga.

Anasema  DCPC   kwa  kushirikiana  na Muungano  wa  clabu za Habari Tanzania(UTPC) wana fomu maalum inayojazwa  ambayo inaeleza  kama  mwandishi amepashida.

“Kupitia hiyo fomu tunaagalia kama ni shida ya haraka tunawasiliana  na chama cha vilabu Tanzania (UTPC) ,baraza la Habari na LHRC  kuona  namna  gani  tunawasaidia.

“Lakini pia tunawafundisha waandishi kuwa afya zao ni  muhimu   kuliko  kitu  chochote  na  akiweza  kulinda  afya  ataweza  kufanyakazi,”anaeleza.

Anasema  kwa  kipindi cha mwaka  jana  waliweza kugawa  vifaa  mbalimbali  vya  kujikinga.

“Kila mwanachama alipata  vifaa  kama  barakoa na vitakasa mikono (sanitizer).

Hata hivyo anasema kwasasa asilimia  kubwa ya waandishi hawachukui  tahadhari  licha ya  jitihada  hizo.

“Wengine ni kwasababu ya chanjo na sio wengi wanaozingatia ni  wachache  mno,”anasema.

Saed Kubenea ni  Miongoni   mwa  wamiliki  wa chombo cha Habari hapa nchini anasema jitihada wanazofanya ni kuwasisitiza  waandishi  wao  kujikinga wanapokuwa kazini.

“Kuhusu  kujikinga  ni  suala la mtu binafsi kama hana mwamko  haiwezi  kusaidia  na pia kwenye media zetu kipindi hiki kumekuwa na mtikisiko wa uchumi hivyo kuwapa vifaa mara kwa mara inakuwa  changamoto.

“Nawashauri  waandishi  wenyewe kwanza wajijali na  kuchukua   tahadhari  wanapokuwa  kazi,”anasisitiza.

MOAT  TUNAANGALI HILI

Wamiliki wa vyombo vya habari wananafasi kubwa kuhakikisha kuwa waandishi wanapata vifaa vya kujikinga na  virusi  vya Corona.

Inagawa ni miongoni mwa majukumu yao lakini Mwenyekiti wa  Wamiliki wa  vyombo  vya  habari  nchini (MOAT) Samwel Nyalla anasema hawawezi kulazimisha hilo  badala  yake  wanajikita  zaidi  katika sera na biashara.

“Hatufanyi  kazi  kwa  command  na hatuingii ndani kwa wawekezaji wako wa aina mbalimbali hivyo sisi tunafanyakazi na wenye vyombo na sio waandishi wa habari lakini ni muhimu kila mwandishi kujali afya yake anapokuwa  kazini,”anasema  Nyalla.

MAMBO YA KUZINGATIA

Soko anasema  Kundi la waandishi lipo katika hatari na linatakiwa  kuchua  hatua  katika  kujikinga.

“Kazi za waandishi ni  kuhabarisha na  kuelimisha  kuhusu covid hivyo waendelee kuwaelimisha jamii kuhusu ugonjwa  huo  pamoja na  kuzingatia  kujikinga,”anaeleza.

Mark anawasisitiza  waandishi  wa  habari  kuwa hakuna habari bora zaidi  ya  maisha yao.

“Ukitoka  kwenye   uandishi  wa  habari  ujue  wewe  ni baba ,mama na unandugu  usipofata  tahadhari utahatarisha maisha yako na hautafikia malengo yako,”anaeleza.

Mkurugeziwa TAMWA Rose Ruben anasema wanaendelea kusisitiza  waandishi  kuchukua  tahadhari.

“Wajilinde  wenyewe  kwani  maisha  niyao na pia wanapojilinda  wanawalinda  na  wengine,”anashauri.

CHANJO NI MUHIMU

Agosti 4, Mwaka  huu  dozi 1,008,400 za chanjo zilikuwa zimesambazwa  kwenye  mikoa yote 26 na  inatolewa kwenye  vituo  zaidi 550  nchi  nzima.

Kwa mujibu  wa  Msemaji  wa  Serikali Gerson Msigwa anasema   jumla  ya  Watanzania  zaidi  ya 345,000 wameshapatiwa chanjo  hiyo na  kazi ya  utoaji chanjo hizo  inaendelea.

Wataalamu wa afya wanasema chanjo ni njia moja wapo ya kujingana  maambukizi  ya  virusivya corona.

Martha Magawa ni miongoni mwa waandishi waliopata chanjo anasema ni muhimu waandishi kupata chanjo kwa hatua  zaidi za kujikinga.

“Serikali  imewapa  kipaumbele kwa  waandishi wa Habari kupata chanjo  tangu  siku  ile  imezinduliwa  na Raisa Samia.

Mjumbe  wa baraza la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Nevvile  Meena,anasema  kundi la waandishi ni  muhimu  kupata  chanjo kwani ni  njia  moja wapo ya kujikinga.

“Kisanyasi chanjo inapunguza watu kupata ugonjwa mkali ambao utawaumiza na uwezekano wa kufa haimaanishi kuwa  hata  kufa.

“Na ukizingatia  waandishi  wa Habari ni  sehemu ya  jamii hatuwezi kukwepa maambukizi na sisi tupo  kwenye hatari,”anaeleza.

Anasema  hatari  huja pale kazi  zao  zinapokuwa za kuchangamana na watu kwani inabidi watoke waende sehemu na  kwenye mikusanyiko.

“Kwa hali hiyo huwezi kuondoa umuhimu wa waandishi wahabari kuchanja hivyo chanjo ni njia moja wapo ya kuzuia  maambukizi,”anasisitiza Meena.

MIKAKATI WA SERIKALI

HabariLEO ilifanya mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya  Afya,Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee  na Watoto, Prof Abel Makubi ambaye anasema waandishi ni kundi ambalo linaangaliwa zaidi na serikali katika kujikinga na virusi pamoja na  kuelimisha  jamii.

“Kwanza kwakutambua umuhimu wa  waandishi  wa Habari serikali ilitoa kipaumbe ya wao kupata chanjo utakumbuka  wakati zoezi  linazinduliwa pale  ikulu na waandishi waliopo walipata chanjo na hii ni njia moja wapo  ya  kujikinga.

“Lakini pia serikali imekuwa ikitoa  mafunzo mbalimbali kwa waandishi kuhusu ugonjwa huo ili na waowaende kuwahabarisha jamii namna ya kujikinga kwani tunawategemea  zaidia  wao,”anaeleza Prof Makubi.

Anasema anawasihi waandishi kuchukua tahadhari wanapokuwa katika  majumu yao na pia kupata  chanjo ya Covid -19 kama  hatua ya  kujikinga.

“Jamii inawategemea na kuwatazama wanatakiwa kuwa mfano mzuri  katika  kujikinga na  kupata chanjo ya corona,”anabainisha.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/c0490fc9324f9e52420632335c1190a5.jpg

MAZAO mengi ya chakula, matunda na biashara kama ...

foto
Mwandishi: Na Aveline Kitomary

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi