loader
Dstv Habarileo  Mobile
Zaidi ya asilimia 80 ya chanjo yatolewa

Zaidi ya asilimia 80 ya chanjo yatolewa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mpaka sasa zaidi ya asilimia 80 ya chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 imetolewa kwa Watanzania.

Serikali iliagiza chanjo milioni moja na kuanza kuzitoa kwa wananchi mwanzoni mwa Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kufungua Kongamano la Tano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jijinji hapa jana, Majaliwa alisema mpaka sasa chanjo zaidi asimia 80 zimetolewa na kuwahimiza wananchi kutumia chanjo kidogo zilizobaki kuchanjwa ili kurutubisha miili yao.

“Tunashukuru tumefikia asilimia zaidi ya 80, tumebakiwa na chanjo kidogo kwenye mikoa, kwa hiyo wananchi tumieni fursa ya kuchanja ili kila mmoja aweze kufikia malengo. Kama bado kutakuwa na mahitaji tutaleta nyingine na lengo ni afya ya Watanzania,” alisema Waziri Mkuu.

“Kuna wanaosema tofauti, lakini maamuzi ni yako mwenyewe kwani suala la afya ni la mtu binafsi,” aliongeza.

Alisema utoaji wa chanjo ni moja ya afua ambazo serikali inazitoa katika kupambana na ugonjwa wa Covid-19.

Aidha, Majaliwa alisema ugonjwa wa Covid-19 upo nchini na umesababisha madhara makubwa kwa baadhi ya ndugu ikiwamo kupoteza maisha na wengine kuendelea kuugua.

“Kwa msingi huo, ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Covid-19. Tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya kuhusu lishe na kufanya mazoezi. Aidha, pale unapoona dalili ambazo huzielewi basi wahi kituo cha kutolea huduma za afya kwa uchunguzi na uangalizi zaidi,” alisema Majaliwa.

Aliongeza, “Naamini sasa elimu inaendelea kutolewa ya namna ya kujikinga na maambukizi, tunaona dalili nzuri, lakini bado tatizo lipo, tuendelee na kujikinga, tuendelee kuwasikiliza wataalamu wetu wa afya, na masharti yote wanayoyatoa ambayo tunapaswa kuyafuata ni muhimu tukafanya hivyo, wakati wote.

Alisema chanjo ni moja afua ya kukabiliana na Covid-19 na kusisitiza kuwa pamoja na serikali kusema chanjo ni hiyari, lakini kuna umuhimu wa kuchanjwa.

“Tumeona mataifa ya wenzetu wako katika nafasi nzuri siku hizi wanaacha hata barakoa kwa sababu kila mmoja amechanja na watu wana uhakika na afya zao, na sisi tungependa tufikie hapo hivyo wengi

wakajitokeza wakachachjwe kwa idai kubwa ili tuwe na uhakika wa kinga ndani ya nchi,” alifafanua.

Aidha, aliwataka wakuu wa mikoa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao umuhimu kwa kuchanja kwa wananchi.

“Niwatoe hofu wananchi wote kuwa chanjo hii ni salama na haina madhara. Chanjo hii pia ni hiari, lakini muhimu kwelikweli katika kupambana na Covid-19.”

Aidha, alisema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi, alisistiza haja ya kila mwananchi kushiriki sensa ya watu na makazi.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi