loader
Israel inamsaka rubani aliyepotea miaka 35 iliyopita

Israel inamsaka rubani aliyepotea miaka 35 iliyopita

Shirika la ujasusi la Israel ‘Mossad’ limeanza kuendesha operesheni maalumu ya kumtafuta rubani wa ndege Ron Arad anayedhaniwa kuuawa.

Ripoti hiyo imetolewa leo na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), na kuwa hayo yamesemwa na waziri mkuu wa taifa hilo.

Imeripotiwa kuwa Luteni kanali Arad alipotea tangu ndege yake ilipoanguka kwenye anga la Lebanon iliposhambuliwa na mabomu mwaka 1986.

Inaelezwa kuwa aliokolewa na vikosi vya Israel, lakini Arad, ambaye alikuwa nahodha, alikamatwa na wanamgambo wa kiislam wa Shia wa Lebanon, Amal.

Aidha, taarifa zinasema mwaka mmoja baadae, Amal walimtoa kwa fidia ili kubadilishana na raia 200 wa Lebanon na wapalestina 450 waliokuwa wanashikiliwa, pamoja na fedha taslim dola za Marekani milioni tatu, na kuwa hata hivyo mazungumzo yalivunjika baada ya Israel kukataa kuwatoa wapalestina kama sharti la kuachiwa kwa rubani huyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/201dc9be4ab9ac3494799b1440adbb9b.jpeg

KAMPUNI ya Qnet imezindua ...

foto
Mwandishi: BBC, London

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi