loader
R. Kelly afungiwa Youtube

R. Kelly afungiwa Youtube

Mtandao wa kijamii wa 'Youtube' umezifungia akaunti za muziki za Mwanamuziki R. Kelly (RKellyTV & RKellyVevo) ikiwa maamuzi ya kwanza kufanyika  tangu kutiwa hatiani kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.

Msanii huyo hatoweza kuzitumia au kufungua akaunti mpya, lakini nyimbo zake kwenye chaneli za watu wengine zitabaki.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwezi msanii huyo kukutwa na hatia ya makosa manane ya unyanyasaji wa kingono ambayo huenda akafungwa kifungo cha miaka 10 jela.

Mwaka 2017 R. Kelly alituhumiwa kufanya unyanyasaji wa kingono kutaka kujaribu kutembea na msichana aliyejitambulisha kwa jina la Aaliyah aliyekuwa na umri wa miaka 13.
Kelly ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa katika biashara ya muziki, miaka ya 1990 na 2000 baada ya kutoa nyimbo zilizokuwa kwenye chati wakati huo za Ignition na I believe I can Fly pamoja na kuuza albamu nyingi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b2c59f190b43d8b63f772c8871f9da12.jpeg

KAMPUNI ya Qnet imezindua ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi