loader
Waziri Uingereza afariki dunia

Waziri Uingereza afariki dunia

BREAKING: Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, James Brokenshire amefariki kutokana na kansa ya mapafu iliyomsumbua kwa zaidi ya miaka mitatu.

Brokenshire 53, alifanyiwa operesheni na kuondolewa uvimbe kwenye pafu lake la kushoto mwaka huu. Kwa zaidi ya miaka mitatu amekuwa katika Hospitali tofauti kupigania uhai wake.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na familia yake ambapo kupitia taarifa hiyo imeeleza kuwa "Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha James Brokenshire amefariki kwa amani akiwa katika Hospitali ya Darent Valley".

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson  amehuzishwa na taarifa hizo, na kusema kuwa  Brokenshire alikuwa mwema,  mwenye uthubutu kufanya maamuzi yenye mabadiliko.

Boris Johnson amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa alikuwa bega kwa bega kupambania uhai wa Brokenshire.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7b1edc2c5a19be68b65db2cb5bdf9ba5.jpeg

KAMPUNI ya Qnet imezindua ...

foto
Mwandishi: DARTFORD, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi