loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dula Mbabe atamba kumpiga Katompa   

Dula Mbabe atamba kumpiga Katompa  

BONDIA Abdallah Pazi ‘Dula Mbabe’ ametamba kumpiga Tshimanga Katompa katika pambano lao lisilo la ubingwa kwenye ukumbi wa PTA Dar es Salaam leo.

Mabondia hao jana walipima uzito tayari kwa pambano hilo la raundi 10. 

Mbabe atapanda ulingoni kupambana na Tshimanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) badala ya Alex Kabangu kutoka huko huko DRC aliyetangazwa awali kupigana naye.

Akizungumzia pambano hilo, Mbabe alisema alifanya maandalizi ya kutosha ya kupigana na Kabangu na siyo Katompa lakini atahakikisha anamgaragaza ili kurudisha imani kwa mashabiki.

"Binafsi suala la kubadilishiwa bondia nimelijua juzi yaani bado siku tatu kabla ya pambano kitu ambacho naona siyo kizuri kwa upande wangu kutokana na maandalizi ya muda mrefu ambayo nimeyafanya yalikuwa ni ya Kabangu.”

“Kabangu nimeangalia anavyocheza katika video zake nyingi na alikuja hapa akacheza na Hussein Itaba hivyo namjua vizuri, ila huyu wa sasa ukweli simjui na amenipa kazi ngumu pamoja na kocha wangu kumtambua mbinu zake ila nitahakikisha natumia mbinu zote kumpiga," alisema Mbabe.

Wengine waliopima uzito ni Cosmas Cheka atakayecheza na Issa Nampepeche, Adam Ngange na Deo Samweli, Juma Misumali dhidi ya Selemani Said.

Ayoub Mwankina dhidi ya Ajemi Amani, Ibrahim Kiboko atakayemvaa Leonard Dedan na Lulu Kayage ataoneshana ubabe na Agnes Kayange.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/98e56840b7ecdfd8a77300f8c6d595d8.jpeg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi