loader
Dstv Habarileo  Mobile
Twiga Stars, Tanzanite moto

Twiga Stars, Tanzanite moto

TIMU za Taifa za soka za wanawake, Twiga Stars na Tanzanite zimefanya kweli katika michuano ya kimataifa iliyochezwa jana.

Wakati Twiga Stars ilitwaa ubingwa wa michuano ya Cosafa baada ya kuifunga Malawi bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa NMB, Port Elizabert, Afrika Kusini, Tanzanite waliifunga Eritrea mabao 2-0 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Twiga Stars ilisubiri hadi kipindi cha pili kupata bao pekee lililofungwa na Enekia Kasonga, akiunganisha mpira uliotemwa na kipa wa Malawi.

Malawi walionesha upinzani mkali kwa Twiga Stars ambao ni timu mwalikwa katika mashindano hayo.

Zambia ndio mshindi wa tatu baada ya kuifunga Afrika Kusini kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 katika dakika 90.

Twiga Stars sasa imeungana na timu za wanawake za U-20 na U-17 kutwaa kombe hilo katika michuano hiyo.

Kocha Bakari Shime ameibuka kocha bora wa mashindano na Amina Bilal mchezaji bora, Sibulele Holweni wa Afrika Kusini mfungaji bora kwa mara ya pili mfululizo na Zambia imekuwa timu yenye nidhamu kutoa kipa bora, Petronela Musole.

Rais Samia Suluhu Hassan aliipongeza Twiga Stars kwa kutwaa ubingwa na kusema ubingwa huu umeleta heshima, kuitangaza nchi na kutia chachu kwa vijana kushiriki michezo.

Pia alilipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na wote walioshiriki kuiandaa timu.

Nayo Tanzanite Queens, katika mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilifanikiwa kufuzu raundi ya tatu kwa kuitoa Eritrea kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya mchezo wa awali kushinda mabao 3-0 mjini Asmara, Eritrea.

Kwa matokeo hayo sasa Tanzanite watacheza na mshindi kati ya Namibia au Burundi na mshindi katika mechi hiyo ndiye atakayefuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Costa Rica mwakani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bcd9946e450f94d5544ed887577cacb5.jpeg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi