loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mashindano ya 'Capital City Marathon' yafanyika Dodoma

Mashindano ya 'Capital City Marathon' yafanyika Dodoma

MASHINDANO ya pili ya Capital City Marathon 2021, yamefanyika jijini Dodoma leo chini ya udhamini wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 2,000 kutoka kila pembe ya nchi.

Wakimbiaji kutoka Arusha na Singida waling’ara katika mbio hizo na kujinyakulia medali na vitita vya fedha taslimu.

Washindi wa mbio za 21km upande wa wanaume ni Josephati Gisemo (01:06:47)-Arusha, Hamisi Athumani (01:06:50) Singida, Yohan Sule (01:07:12) Arusha, Aloyce Simbo , Agustine Sule, Rashid Muna, Marco Joseph,  Emmanuel Gadiye, Saidi Juma na Nestory Stivin .

Washindi upande wa wanawake, Mshindi Matanga (01:20:59), Mery Naali (01:23:02), Tunu Andrea (01:23:11), Sara Ramadhani, Angel John, Ramla Phabian, Asia Dedu, Visa Mhalwa, Rose Malia na Shania John.

Washindi wa 10km wanaume ni Kaposh Laizer (29:03:16), Inyasi Sule (29:11:93) , Fabian Nelson (29:51:23), Jamali Saidi, Nelson Mbuya, Haji Luli, Elizante Elibariki, Shija Ngelela, Amani Owen na  Bosco Kangalwe.

Washindi wa 10km wanawake ni Transfora Musa (34:04:02), Anastazia Dolomogo (35:32:23), Aisha Lubuna (35:53:91), Neema Kisuda, Agnes Protas, Rebeca Bajuta, Neema Sanka, Sarah Hijti, Anna Rogath na Aisha Mohamed.

Akizungumza leo mara baada ya kukamilika kwa mbio hizo, mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema mbio hizo zimeunga mkono jitihada za serikali za katika adhma yake ya kuhakikisha inapiga vita magonjwa yasiyo ya kuambukiza .

"Nashukuru kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye anasisitiza wananchi kufanya mazoezi , niwaombe kila mmoja wetu akawe balozi huko tunakotoka, matukio haya yanapokuwepo mahali yanafanya mambo mengi ikiwemo lile la afya kwa sisi tuliofanya mazoezi ’’ amesema

Kwa upande wake , Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC)  Yessaya Mwakifulefule ,amesema mbio hizo ni mbio ambazo hupanda thamani kila mwaka hivyo husaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza ajira kwa vijana .

‘’NIC tumedhamini mbio hizi kupitia bidhaa yetu ya Bima ya Makazi  tukiwataka watanzania waweze kulinda makazi yao , hii si mara ya kwanza kwa NIC kushiriki kwenye michezo mbalimbali kwa maana ya riadha, mpira wa miguu, kwasababu tunaamini michezo ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na hata serikali yetu inasisitiza kwamba vijana wajiajiri kupitia michezo’’ amesema

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo Nsolo Mlozi, amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika kufanikisha mazoezi na mazoezi kwani imeweza kurahisisha maisha ya watanzania kwa kujenga undugu pamoja na urafiki’’ Leo tuko hapa watu takribani elfu mbili maana yake Dodoma imejengeka kiuchumi’’

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/dfd4c202ee55b68af7e180b476ad47f8.jpeg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi