loader
CCM yampongeza Rais Samia vita ya ubaguzi

CCM yampongeza Rais Samia vita ya ubaguzi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais Samia Suluhu kwa kuendelea kupinga ubaguzi wa aina zote katika uongozi wake tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miezi sita iliyopita.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamidu amewaambia waandishi wa Habari Mjini Dodoma Oktoba 12 kwamba  Rais Samia amekuwa kipaumbele katika kulinda haki, usawa, na kupambana na unyanyasaji wa aina zote nchini.

“Ameendelea kuonyesha kuwa Taifa letu halifungamani na dini yoyote, kupinga unyanyasaji na udhalilishaji wa aina zote,” amesema Shaka.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amepongezwa kwa kufanikisha mkopo wa Tsh trilioni 1.3 kutoka Benki ya Dunia ambao utafanikisha ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu na afya.

Pongezi hizo zimetolewa leo Oktoba 12, 2021 na Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kupitia kwa katibu mwenezi wa chama hicho, Shaka Hamidu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Shaka amesema Rais Samia ameigusa jamii hasa katika kipindi hiki cha janga la UVIKO-19 ambapo, licha ya juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Serikali itaendelea kuwafariji watanzania kwa kujenga miradi mbalimbali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f2bfe6159a82417113934ce28379ad89.jpg

UCHUMI na maendeleo ni mambo yanayohitaji kujengewa miundombinu ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi