loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kapombe awashukuru madaktari Simba

Kapombe awashukuru madaktari Simba

Beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe ameishukuru timu ya madaktari wa klabu hiyo kwa kumsaidia kupona haraka maumivu ya nyama za paja. 

Akizungumza hivi karibuni Kapombe amesema kwa sasa yupo fiti na ameshaanza mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana. 

"Nawashukuru madaktari kwa huduma ambayo wamenipatia na kunifanya nipone haraka hivi sasa nipo sawa na tayari nimeanza mazoezi nawenzangu," amesema Kapombe. 

Daktari mkuu wa Simba Yassin Gembe ndiye aliyeshirikiana na jopo la madaktari wenzake kuhakikisha Kapombe na wachezaji wengine majeruhi wanarudi haraka uwanjani. 

Beki huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars ' amesema kwa sasa anajifua kwa nguvu ili kuhakikisha anakuwa timamu kwa ajili ya pambano lao la Ligi ya Mabingwa wiki ijayo. 

Beki huyo ambaye kwa sasa ni nahodha msaidizi wa timu hiyo amekosa mchezo mmoja dhidi ya Dodoma Jiji ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Imeandaliwa na Mohamed Akida

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/fc00d58ea2bf3631cb11e0e48f396fd9.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Na Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi