loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kocha: Nina imani kubwa na Mayele na Makambo, tulieni

Kocha: Nina imani kubwa na Mayele na Makambo, tulieni

KOCHA Mkuu wa Yanga Nasriddine Nabi amesema licha ya washambuliaji wake kuanza msimu wakiwa chini lakini imani yake juu yao ni kibwa.

Katika mechi mbili za ligi kuu ambazo Yanga imecheza imefunga mabao mawili na yote yamefungwa na viungo na siyo washambuliaji wake tegemezi Fiston Mayele na Heritier Makambo.

Akizungumza na mtandao huu Nabi amesema hana shaka na uwezo waliokuwa nao wawili hao ispokuwa ugeni wa ligi ndio unawasumbua ingawa baada ya muda mfupi kila kitu kitakaa sawa kwao.

"Hawa ni washambuliaji waviwango kila mtu anajua hilo sababu walishathibitisha ubora wao tangu huko walikokuwa sasa kutofunga mabao kipindi hiki hakiwezi kuwa sababu ya kuwaona hawafai kinachowakuta mchezaji yeyote duniani kinaweza kumtokea hivyo mashabiki wawe watulivu," amesema Nabi.

Kocha huyo amesema kitu kingine kinachosababisha wachezaji hao kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ni kukutana na wachezaji tofauti na wale ambao wamezoeana nao hivyo bado hawaja elewana vizuri.

Mayele amejiunga naYanga msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo na mpaka sasa ameifungia bao moja tu timu yake kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba huku Makambo bado akipambana kufungua akaunti yake ya mabao.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0db6b1ed9bd3a8b89d173d807a1c659e.jpg

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi