loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk Mwinyi: Tuzo ya Nobel k Mwinyi: Tuzo ya Nobel fahari kwa Watanzania

Dk Mwinyi: Tuzo ya Nobel k Mwinyi: Tuzo ya Nobel fahari kwa Watanzania

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema tuzo ya Nobel katika Fasihi aliyoipata Mtanzania, Profesa Abdulrazak Gurnah (73) ni fahari kwa Wazanzibari, Watanzania na Waafrika kwa ujumla.

Dk Mwinyi alisema hayo wakati akizungumza na Profesa Gurnah kwa njia ya mtandao kumpongeza. “Nichukue fursa hii vilevile nikukaribishe uje Zanzibar sehemu ambayo ndipo ulipozaliwa, ndio nyumbani.

Kwa hiyo sisi kwa sababu tunajifaharisha kwa mafanikio yako basi tunaona ni vizuri tukupe mwaliko rasmi ukipata wasaa wakati wowote basi karibu sana nyumbani,” alisema.

Profesa Gurnah (pichani) alimshukuru Dk Mwinyi kwa kuzungumza naye na kumkaribisha nyumbani. Mwandishi huyo wa riwaya amekuwa mshindi wa kwanza Mtanzania katika tuzo za fasihi na wa pili kutoka Afrika. Riwaya iliyompatia tuzo ilihusu athari za ukoloni na hatma ya wakimbizi katika ghuba baina ya tamaduni na mabara.

Tuzo hiyo ilitolewa na taasisi ya Uswisi ya Nobel na ina thamani ya fedha ya corona za Uswisi milioni 10 sawa na Dola za Marekani milioni 1.14. Profesa Gurnah alizaliwa Zanzibar na aliwasili na kuishi Uingereza miaka ya 1960 akiwa mkimbizi. Hasi sasa ameandika riwaya 10 na hadithi kadhaa fupi fupi. Alikuwa Profesa wa Kiingereza na fasihi baada ya uhuru katika Chuo Kikuu cha Kent, Canterbury, hadi alipostaafu.

Hakuna mwandishi yeyote wa fasihi mweusi aliyewahi kushinda tuzo hiyo tangu aliposhinda Wole Soyinka mwaka 1986. Kitabu chake cha riwaya cha nne alichoandika kiliingia kwenye orodha ya kuwania tuzo ya Booker mwaka 1994.

Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hiyo ya Nobel alisema Gurnah kupitia kitabu chake cha Memory of Departure alielezea ufafanuzi wa ubaguzi na kuweka wazi Afrika Mashariki yenye watu mbalimbali ambayo wengi katika maeneo mengine ya dunia hawaifahamu.

“Kujitolea kwa Abdulrazak Gurnah kuzungumzia ukweli na kutopenda urahisishaji ni jambo lililovutia na kufurahisha,” alisema.

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi